Kuna manunguniko kuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe ana mkonp katyi akufungwa kwa Jambo Forums. Je hili lina ukweli kwa kiasi gani?

Kuna watu wanasema kuwa waziri huyu ambaye ana sifa za hasira amekuwa akilalama jinsi gani alivyohusishwa na maneno ambayo hatuna ukweli nayo kuwa anagombania tenda ya vitambulisho vya Taifa na Sumaye.Je kuna ukweli gani kwenye hili?

rais_na_membe.jpg

Kwa nini website ifungwe baada ya wazalendo kumvalia njuga waziri huyu na rafikiyake bwana MWIKALO??

Advertisements

Members wawili wa JAMBO FORUMS wamekamatwa sasa chukueni nafasi hii kuuelezea ulimwengu jinsi jani serikali yetu inavyo wanyima watu uhuru wa kujieleza hapa:

Shukurani za dhati kwa Mwanakiiji na Michuzi blog

KUTOKANA NA MWANAKIJIJI…..

 

Habari ambazo zinazidi kutiririka kuifikia KLH News zinaonesha kuwa vijana waliowekwa kizuizini kwa karibu masaa 24 wanadaiwa kuhusika na mambo mengi ambayo mlolongo wake unaweza kupita hadithi za Alfu Lela Ulela. Baadhi ya madai yanayotajwa ni pamoja na wao ku”hack” kompyuta za serikali, kuendesha tovuti inayotukana viongozi, kuendesha tovuti yenye mambo ya ngono, kuvujisha siri za serikali.Baadaye Jumatano inatarajiwa kuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini Bw. Robert Manumba atazungumzia sakata hilo la vijana hawa akichagua mojawapo ya makosa ambayo wamekuwa wakiyatafuta dhidi yao. Kuna uwezekano mkubwa vijana hao kuhusishwa na tovuti ya JF kuwa inakashfu na kukejeli viongozi wakubwa wa serikali. Vijana wametakiwa kuripoti makao makuu ya Polisi majira ya kama saa tatu asubuhi.

Hata hivyo vyanzo vingine karibu na kuta za vyombo vya usalama vinaonesha kuwa jambo hili linawahusisha kwa namna fulani watu wa Usalama wa Taifa hasa baada ya chombo hicho nyeti kuhusishwa na vitendo vya ufisadi nchini. Itakumbukwa kuwa kwenye jambo forums kulikuwa na mada iliyokuwa inaakisi maneno ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Bw. Daud Balali kuwa fedha zilizolipwa kwa Kagoda Agriculture zilikuwa ni kwa ajili ya Usalama wa Taifa.

Hadi hivi sasa chombo hicho hakijakanusha kuhusika kwake na sakata hilo la Benki Kuu.

Wachunguzi wengine wa mambo ya kisheria wameiambia KLHN kuwa zile sheria ambazo zilidhaniwa kuwa zimekufa zinaweza kuibuliwa kwenye sakata hili na kina Manumba. Sheria ambayo inaogopwa sana ni ile ya Usalama wa Taifa ya 1970, ile ya magazeti ya 1976 na sheria mpya iliyounda TISS (Idara ya Kijasusi) ya 1996.

Endapo Sheria hizo zitatumiwa kuna uwezekano kuwa uhuru wa kutoa na kupata habari nchini utawekwa kizimbani kwa namna ya pekee ambapo teknolojia ya kisasa ya kiintaneti inaweza kuwa ni upande wa mashtaka na utetezi kwa wakati mmoja. Sheria hizo zote tatu zinapatikana kwenye “Pics and Docs” hapo juu kwa yeyote anayependa kuzifuatilia.

jf.jpg