Members wawili wa JAMBO FORUMS wamekamatwa sasa chukueni nafasi hii kuuelezea ulimwengu jinsi jani serikali yetu inavyo wanyima watu uhuru wa kujieleza hapa:

Shukurani za dhati kwa Mwanakiiji na Michuzi blog

KUTOKANA NA MWANAKIJIJI…..

 

Habari ambazo zinazidi kutiririka kuifikia KLH News zinaonesha kuwa vijana waliowekwa kizuizini kwa karibu masaa 24 wanadaiwa kuhusika na mambo mengi ambayo mlolongo wake unaweza kupita hadithi za Alfu Lela Ulela. Baadhi ya madai yanayotajwa ni pamoja na wao ku”hack” kompyuta za serikali, kuendesha tovuti inayotukana viongozi, kuendesha tovuti yenye mambo ya ngono, kuvujisha siri za serikali.Baadaye Jumatano inatarajiwa kuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini Bw. Robert Manumba atazungumzia sakata hilo la vijana hawa akichagua mojawapo ya makosa ambayo wamekuwa wakiyatafuta dhidi yao. Kuna uwezekano mkubwa vijana hao kuhusishwa na tovuti ya JF kuwa inakashfu na kukejeli viongozi wakubwa wa serikali. Vijana wametakiwa kuripoti makao makuu ya Polisi majira ya kama saa tatu asubuhi.

Hata hivyo vyanzo vingine karibu na kuta za vyombo vya usalama vinaonesha kuwa jambo hili linawahusisha kwa namna fulani watu wa Usalama wa Taifa hasa baada ya chombo hicho nyeti kuhusishwa na vitendo vya ufisadi nchini. Itakumbukwa kuwa kwenye jambo forums kulikuwa na mada iliyokuwa inaakisi maneno ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Bw. Daud Balali kuwa fedha zilizolipwa kwa Kagoda Agriculture zilikuwa ni kwa ajili ya Usalama wa Taifa.

Hadi hivi sasa chombo hicho hakijakanusha kuhusika kwake na sakata hilo la Benki Kuu.

Wachunguzi wengine wa mambo ya kisheria wameiambia KLHN kuwa zile sheria ambazo zilidhaniwa kuwa zimekufa zinaweza kuibuliwa kwenye sakata hili na kina Manumba. Sheria ambayo inaogopwa sana ni ile ya Usalama wa Taifa ya 1970, ile ya magazeti ya 1976 na sheria mpya iliyounda TISS (Idara ya Kijasusi) ya 1996.

Endapo Sheria hizo zitatumiwa kuna uwezekano kuwa uhuru wa kutoa na kupata habari nchini utawekwa kizimbani kwa namna ya pekee ambapo teknolojia ya kisasa ya kiintaneti inaweza kuwa ni upande wa mashtaka na utetezi kwa wakati mmoja. Sheria hizo zote tatu zinapatikana kwenye “Pics and Docs” hapo juu kwa yeyote anayependa kuzifuatilia.

jf.jpg


  1. Wasilinana na Mwanakijiji na mwambie aache kuchezea maisha ya wenzake. Aache haraka sana tafadhali. Anachoandika kina athari kwa wenzake. Mimi mzalendo halisi

  2. Mlalahoi

    Achana na upuuzi huo,fisadi UNKNOWN (well,you can pretend to be unknown but we surely know that wewe ni FISADI).Mwanakijiji wembe uleule,watabana mwishowe wataachia

  3. Anonymous

    hakuna kulala hawa ndio mafisadi wanatafuta jinsi ya kunyamazisha wa tz

  4. mtuwapwani

    Tatizo hao maafisa usalama bado washamba sasa wanafatilia Jf ili iweje ikifungwa Jf watu watafungua nyengine na itakua kali zaidi ya jf..hao wana usalama akili hawana kabisa na wataona maana sisi wengine tupo iraqi tunauwezo wa kufanya lolote bila kudhuriwa na upuuzi wao

  5. mtanganyika

    Waugwana hawa wanaojifanya ndio sources za habari kutoka Tanzania tuwe macho nao.
    tunapatikana pia kwenye jamboforums.blogspot.com kwa muda huu.

  6. jmushi1

    We surely do miss jf..lakini i believe victory will eventuall be on the freedom side!

  7. Bongosamurai

    Hima wana-JF hanyamazishwi mtu hapa, ukweli unauma sana na Tanzania siyoongozwa na MAFISADI inawezekana.Enzi ya MAFISADI iko mwishoni ama zao ama zetu..!

  8. wikendi njema

    Nashauri tushitaki kwenye vyombo vya habari vya kimataifa

  9. Inasikitisha sana jinsi Ufisadi Unavyoitafuna nchi yetu Tanzania,Sidhani tena kama kauli ya kumuhenzi baba wa taifa itatumika tena October 10,2009. waatakao tumia kauli hiyo itabidi wawe makini na watakayoyazungumza




Leave a Comment